Amos 8:2-7

2 aAkaniuliza, “Amosi, unaona nini?”

Nikajibu, “Kikapu chenye matunda yaliyoiva.”

Ndipo Bwana akaniambia, “Wakati umewadia kwa watu wangu Israeli; sitawahurumia zaidi.”

3 b Bwana Mwenyezi asema, “Katika siku ile, nyimbo katika Hekalu zitageuka kuwa maombolezo. Miili mingi, mingi sana: itatupwa kila mahali! Kimya!”
4 cLisikieni hili, ninyi ambao mnawagandamiza wahitaji,
na kuwaonea maskini wa nchi,

5 dmkisema, “Ni lini Mwezi Mwandamo utakapopita
ili tupate kuuza nafaka,
na Sabato itakwisha lini
ili tuweze kuuza ngano?”
Mkipunguza vipimo,
na kuongeza bei,
na kudanganya kwa mizani zisizo sawa,

6 emkiwanunua maskini kwa fedha,
na wahitaji kwa jozi ya viatu,
na mkiuza hata takataka za ngano
pamoja na ngano.

7 f Bwana ameapa kwa kiburi cha Yakobo: “Kamwe, sitasahau chochote ambacho wamefanya.
Copyright information for SwhKC